Migogoro baina ya jamii zilizoko Tana River, imezua hali ya wasiwasi siku za hivi karibuni, wakaazi wakikimbilia kutoka makazi yao na kwenda sehemu zengine zilizo salama.
Wakaazi wa eneo hilo wanasema kwamba, migogoro hii ya mara kwa mara imehusishwa hasa na mizozo ya ardhi pamoja ukabila katika eneo hilo. Wanaiomba serikali kungilia kati na kuleta sulu ya kudumu katika eneo lote la Tana Delta.
Viongozi wa jamii hizi, viongozi wa dini, wakaazi pamoja na viongozi wa serikali walikutana Tarassa katika Parokia ya Tarassa katika kanisa Katoliki la Tarassa chini ya uongozi wa Baba Paroko Fidel Machara ili kuzungumza na kuleta upatanisho baina ya jamii hizo. Padre Fidel Machara vilvile ni mwanachama wa CICC, Coast Inter-faith Council of Clerics Tana Delta.
Mhashamu Baba Askofu Willybard Lagho, askofu wa jimbo katoliki la Malindi ambaye pia ni mwenyekiti wa Tume ya Majadiliano Baina ya Dini na Uekumene (CIRDE) alihudhuria mutano huo.
Wakaazi wanoishi Tana River wanakumbwa na matatizo mbalimbali ikiwemo, kutopata vitambulisho vya kitaifa kwa wakati, mkanganyiko wakati wa kutafuta vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wao miongoni mwa stakabadhi zengine muhimu za serikali.
Mikutano ya mara kwa mara imefanyika katika eneo la Minjila, Tarassa na tana Delta kwa ujumla ila wakaazi wanalalamika kwamba inachukua muda mrefu kusaidikia na hata kupata suluhu la kudumu.
Katika mkutano huo uliojumuisha vingozi mbalimbali pamoja, wakaazi walipewa fursa ya kueleza chanzo cha malumbano yao a mara kwa mara kwa mara katika eneo hilo.
“Tumekuwa na kikundi amabacho kimekuwa na jukumu la kuzunguka nyanjani na kutambua matatizo yanayowakumba na kufanya vikao na wakaazi, kuwaelimisha na kuhakikisha wanaishi kwa amani. Wakaazi wa Chara, Handaraku, na sehemu zenigine za Tana Delta wamekumbwa na mafuriko kila kunaponyesha mvua, na walihimizwa kuenda sehemu ya juu na walipohamia huko kukawa na hali vurugu kwa jamii zinazoishi huko na zile zilizohamia huko. Tulifuatilia na kutatua tatizo hilo ila bado matatizo ninmengi ambayo yanatukumba,’’ alisema mmoja wa viongozi wa jamii huku Tarassa.
Mkaazi mwengine alisema kwamba tatizo la maji limewakumba kwa muda mrefu sana ikiwalazimu kusafiri kilomita nyingi kutafuta maji. Aliongezea kuwa kila wanapopanda inakuwa changamoto kwani kunazio jamii ambao ni wafugaji wa mbuzi, ng’ombe, kondoo na punda, ambao wanafuga wanyama wengi na mara na shambani na kula mimea hiyo.
“Nilitembelea mahali wanakoishi wakazi hawa na ni hali duni sana na wanapitia matatizo makubwa sana. Tuwe na utaratibu flani unaotambulika na viongozi wenu kila wakati kuhusu maswala ya ardhi. Tusisitize swala la elimu kwa watoto wetu kwani litapanua mawazo ya watoto wetu na kuwapatia njia mbadala ya kujimudu katika maisha kwasababu si kila mtoto ategemea ukulima. Tusipothamini elimu, watoto wetu watabakia pale pale ambapo tumezaliwa na tunajitafutia shida kubwa,’’ alisema Baba Askofu.
Vilevile Askofu Lagho aliwaonya dhidi ya kuuza mashamba yao na kuwahimiza kutumia ardhi zao kwa kilimo na kupata fedha za kujikimu kimaisha. Aliwahimiza kushirikiana na viongozi wao pamoja na wale wa serikali ili kudumisha amani na kuleta maendeleo katika eneo lao.