Siku ya Wanawake Ulimwenguni (International Women's Day) huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi.
Siku hii inatoa fursa ya kutambua na kusherehekea mafanikio ya wanawake katika nyanja mbalimbali, kama vile siasa, biashara, sayansi, sanaa, na jamii kwa ujumla. Pia ni siku ya kutafakari na kuhamasisha hatua za kuongeza usawa wa kijinsia na kupigania haki za wanawake duniani kote.
Kila mwaka, Siku ya Wanawake Ulimwenguni ina kauli mbiu maalum inayolenga kuhamasisha mabadiliko na kukuza usawa. Ni siku muhimu kwa wanawake na wanaume kushirikiana katika kujenga jamii yenye usawa, haki, na fursa sawa kwa wote.
Wanawake katika dekania ya Watamu ambazo ni Parokia tatu, Msabaha, Mida na Watamu, walijumuika kuadhimisha siku hii. Kina mama hawa walikutana Marian Shrine, Msabaha.
Kina mama walijitokeza kwa wingi wakiongozwa na Padri David Muge ambaye ni msimamzi wa dekania hiyo. Mapadri wengine waliojumuika nao ni Padri Boniface na Padri Joshua Mutuku amaye ni Paroko wa Parokia ya Msabaha.
Misa ya siku hiyo iliongozwa na Padri Boniface ambaye ndiye msimamizi wa kina mama katika dekania ya Watamu. Mapadri wamewashauri kina mama kuyatilia maanani majukumu yao katika familia zao, jamii, Kanisa na shirika lao la CWA. Kina mama ni nguzo muhimu katika kuzijenga familia na jamii zetu.
Siku ya Wanawake Ulimwenguni ina umuhimu mkubwa kwa sababu inatoa fursa ya kutambua na kuadhimisha mchango wa wanawake katika jamii na dunia kwa ujumla. Hii ni baadhi ya sababu zinazoifanya kuwa muhimu.
Kwa ujumla, Siku ya Wanawake Ulimwenguni ni muhimu kwa sababu inatoa jukwaa la kuchochea mabadiliko, kusherehekea mafanikio, na kuhamasisha usawa wa kijinsia na haki kwa wanawake katika jamii zote.