slider10.jpg
slider5.jpg
slider8.jpg
slider6.jpg
slider11.jpg
slider9.jpeg
previous arrow
next arrow

Ningependa kutoa shukurani zangu kwa Wakristu wote, wa Dekania ya Kaskazini, Kusini na Kati. Asante kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki wote kutoka Jimbo la Malindi na pia kutoka Majimbo mengine waliojiunga nasi siku ya Jumapili ya tarehe 05/12/2021 na kutuwezesha kuchangisha fedha nyingi sana kuzidi yote iliyochangishwa miaka mingine iliyopita.

Fedha hizi zitatuwezesha kuindeleza Jimbo letu la Malindi na pia kuanzisha miradi mbali mbali za kunufaisha watu wetu. Ningependa kuwashukuru ninyi haswa kwa kujitolea wakati huu mgumu wa COVID 19, wakati ambapo dunia inapitia janga kubwa kuwahi kutokea. Natumai kwamba Mwenyezi Mungu atatuwezesha tena ili tujitokeze tutakapohitajika mara nyingine kusaidia kulijenga kanisa la Bwana. Mwakani, tutakua na Harambee ya kuchangia mfuko wa Jimbo Tarehe 05/11/22. Kujitokeza kwa Wakristu, ndugu na Jamaa kwa wingi ni ishara tosha kwamba sasa Wakristu wamekubali Kanisa ni lao na kukubali kuchukua jukumu la kuliendeleza. Mwaka ujao tunamwomba Mola atuwezesha tujitokeze tena ili tuchangie mfuko huo wa maendeleo. Nawatakieni heri njema ya Krismai na niseme tu, Asanteni sana'. Askofu Willybard Kitogho Lagho, Askofu wa Jimbo La Malindi. Tusikilize sauti ya Baba Askofu.