Catholic Diocese Malindi

slider10.jpg
slider5.jpg
slider8.jpg
slider6.jpg
slider11.jpg
slider9.jpeg
previous arrow
next arrow

Fumbo la Utatu Mtakatifu. Ni sherehe kati ya sherehe za Bwana ambayo huadhimishwa Dominika inayofuata mara baada ya Pentekoste. Mama Kanisa ameweka sherehe hii baada ya Pentekoste kwa sababu anajua tayari fumbo zima la Utatu Mtakatifu limekwishafunuliwa na kufundishwa kwa kina na Mama Kanisa. Na kwa namna hiyo Mama Kanisa anatushirikisha furaha ijayo kwetu kila siku kwa njia ya Utatu Mtakatifu. Anatushirikisha fumbo la Mungu kukaa nasi daima mpaka ukamilifu. Kwa njia ya fumbo hili upendo wa Mungu kwa wanadamu unafunuliwa hatua kwa hatua mpaka ukamilifu wake.

🥀 Mpendwa, Fumbo la Utatu Mtakatifu kwa kawaida ni fumbo kuu kati ya mafumbo makuu matatu, yaani fumbo la Ekaristi Takatifu na umwilisho, fumbo la neema za Mungu na Utatu Mtakatifu ambao ndio tunasherehekea leo. Ni fumbo ambalo si rahisi kulielewa kwa undani na ukamilifu wake kwa maana ndiyo Mungu mwenyewe.

🥀 Tunachotambua ni kuwa Mungu Baba ni muumbaji, na alipokwisha kuumba mbingu na nchi alimtuma Mwanae ili aokoe mwanadamu aliyepoteza uzuri aliokabidhiwa na Mungu Baba na hivi Mungu Mwana ni Mkombozi.
 
🥀Mwana alipokwisha kufundisha na kumaliza kazi yake kabla ya kupaa mbinguni alihaidi kumpeleka Roho Mtakatifu  mfariji na mwalimu atakayetukumbusha yote na tena hatafanya kinyume na yale yaliyofundishwa na Bwana. Kumbe, Utatu Mtakatifu ni Mungu mmoja lakini nafsi tatu zisizogawanyika, yaani Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Kutambua na kujaribu kuelewa tunahitaji kuwa na imani thabiti.