slider10.jpg
slider5.jpg
slider8.jpg
slider6.jpg
slider11.jpg
slider9.jpeg
previous arrow
next arrow

Mhashamu Baba Askofu Willybard Lagho aliandamana na Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Askofu Philip Anyolo, na kutembelea mradi wa Stella Maris huko Watamu. Huu ni mradi wa jimbo katoliki la Malindi.

Mradi huu ambao uko katika hatua za ujenzi, pindi utakapo kamilika, utakuleta kipato katika jimbo katoliki la Malindi na pia kuwapa ajira waktristu, wale wasio wakristu pamoja na wakaazi wa Watamu.

Askofu Mkuu Philip Anyolo alieleza furaha yake alipotembezwa na Baba Askofu Willybard Lagho katika mradi huo. Alimpongeza Askofu Willbard Lagho na Wakristru kwa ushirikiano wao na kushikana mkono katika kufanikisha mradi huo na pia alisema kwamba ushirikiano huu utaleta mafanikio makubwa jimboni. Askofu mkuu Philip Anyolo kwa furaha alisema kwamba anayo imani kwamba makubwa na mazuri yatafanyika.

Askofu mkuu alisisitiza umuhimu wa ushirikiano na pia akawahimiza wakristu Kuendelea kuwa na moyo huo huo wa kushirikiana na Askofu Willybard Lago.

“Nina furaha kubwa sana kufika hapa Watamu na kujionea mwenyewe mradi huu wa jimbo katoliki la Malindi. Pongezi Askofu Willybard Lagho kwa hii hatua ni nzuri sana na pia Wakristu wakatoliki wamefanya jambo kubwa sana kwa kushirikiano. Tunapokuwa na ushirika mwema basi mambo mazuri huja. Kama vile wanafunzi wa Yesu Kristu walivyoshirikiana katika kueneza injili, basi nyinyi mshirikiane kufanikisha miradi ya jimbo lenu.”