Catholic Diocese Malindi

slider10.jpg
slider5.jpg
slider8.jpg
slider6.jpg
slider11.jpg
slider9.jpeg
previous arrow
next arrow

NURU YENU IANGAZE: Tafakari ya siku;Jumamosi trh 15/7/2023. Na Pd. Carilus OFM. Kumb. ya Mt. Bonaventura, Askofu na Mwalimu wa Kanisa. Mwa.49:29-33;50:15-25,
Mt.10:24-33
"Msiogope basi, bora nyinyi kuliko mashomoro wengi." Ndugu wapendwa nini kinachokufanya uwe na hofu, uogope?Na katika hofu yako unapata faraja wapi? Ndugu zake Yusufu wanahofu kwa sababu ya maovu waliomtendea. Wanafikiri kuwa baada ya kifo cha Baba Yao, Yusufu atalipa kisasi na kuanza kuwatesa.

Badala yake Yusufu anawatuliza na kuwafariji kuwa wasiogope maana wao walikusudia mabaya bali Mungu aliyakusudia kuwa mema ili itokee kuokoka taifa kubwa. Yesu anatambua kuwa mitume wake wanaogopa kwa yatakayowapata katika utume wao na anawatia nguvu na kuwafariji kuwa wasiogope maana Mungu anawajua na atakayemkiri mbele ya watu naye atamkiri mbele ya Baba aliye mbinguni. Ndugu zangu mwizi hukimbia hata kama hakuna anayemfuata. Ndivyo ilivyokuwa na Ndugu zake Yusufu. Leo unaalikwa kutafakari nini kinachokufanya uogope kila mahali. Ni kwa sababu ya maovu yako au kwa sababu ya kutenda mema. Hongera kama unaogopa kwa sababu unatenda mema na wanaokuzunguka wanachukia hilo. Yesu anatuhakikishia wewe ni wa thamani, atakulinda. Lakini ole wako kama unahofu kwa sababu ya maovu yako kama Ndugu zake Yusufu. Yaani unadhani kila mtu ni muovu kama wewe na wanaweza kukutendea maovu. Unapomtendea mtu mwema jambo baya kama walivyofanya Ndugu zake Yusufu je umejua yanayokungoja kesho?Ndugu zangu, tuwe na moyo kama ya Yusufu wa kusema yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Uone uovu unayotendewa kuwa ni fursa anayotumia Mungu kukuinua na kuwainua na wengine. Usiwe na roho ya kisasi bali uwaombee na maadui zako, uwafariji wakati Mungu amekubariki zaidi yao. Nawe leo Sikia maneno yake Yesu usiogope unapotenda mema. Mt Bonaventura utuombee. Na Mungu Mwenyezi awabariki kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. amina. na nuru YENU IANGAZE.