slider10.jpg
slider5.jpg
slider8.jpg
slider6.jpg
slider11.jpg
slider9.jpeg
previous arrow
next arrow

*MAISHA YA WATAKATIFU*

*MT. TOMA WA VILANOVA,* ASKOFU
( 22 SEPTEMBA )

Toma alizaliwa Hispania, mwaka 1438. Alipokwisha timiza umri wa miaka saba, alipelekwa kila siku darasani ili aanze kusoma. Kila mara alipokuta njiani mtoto maskini mwenye njaa, alimpa au chakula chake au nguo yake moja, kwani alikuwa akikumbuka kwamba maskini ndiyo maungo ya Yesu Kristo. Mama yake, alipopata habari hizo, akaanza kumwongezea vyakula mwanawe ili apate kuendelea kutenda matendo ya huruma, pasipo kupungukiwa.

Kisha kumaliza masomo ya chuo kikuu cha Alkala (Hispania), alikuwa mwalimu wa Falsafa. Alipokuwa na umri wa miaka thelathini, akaingia katika Shirika la Wamonaki wa Mt. Augustino, akapewa Upadre. Kwa mahubiri na mafundisho yake, aliwaongoa wakosefu wengi.

Papa alimfanya Padre Toma awe Askofu wa Valensia (Hispania). Mapadre wenzake waliojua ya kuwa hakuwa na kitu, walimpa fedha kiasi, apate kulitengeneza jumba lake na kulinunulia vyombo. Lakini Askofu akaitumia fedha ile yote kwa ajili ya huduma kwa wagonjwa hospitalini. Kila siku, alikuwa akiwapokea mezani kwake maskini, na kuwapa chakula. Kama hawakuweza kufika kwake kwa sababu ya kuwa wagonjwa, yeye mwenyewe alikwenda kuwatazama nyumbani kwao. Wenye madeni aliwapa fedha za kulipia; watoto na wagonjwa wote aliwatunza kwa upole na upendo. Alipozimia roho, mwaka 1555, alikuwa hana kitu chochote, hata kitanda alichokuwa akilalia hakikuwa chake, alikuwa amekiazima kwa jirani zake. Papa alimtaja Mtakatifu mwaka 1658.

*MT. TOMA WA VILANOVA, UTUOMBEE*

*MASOMO YA MISA*

I. 1 Tim. 6:2-12

Zab. 49:5-9,16-19

INJILI. Lk. 8:1-3