Catholic Diocese Malindi

slider10.jpg
slider5.jpg
slider8.jpg
slider6.jpg
slider11.jpg
slider9.jpeg
previous arrow
next arrow

*MAISHA YA WATAKATIFU*

*MT. PAMBO,* MKAA PWEKE
( 17 JULAI )

Inasemekana kuwa Pambo alizaliwa huko Misri, na katika ujana wake aliwahi kuwa mfuasi wa Mt. Antoni mkaa pweke jangwani huko Misri. Alisisitiza kufanya kazi kwa mikono, kwa desturi alisuka mikeka kutokana na majani ya michikichiki. Alifunga na kusali kwa muda mrefu. Zoezi kubwa hasa alilofanya katika maisha yake ni kuutawala ulimi wake kukaa kwa kimya na kufikiri kwanza kabla ya kusema. Wakati mwalimu wake alipompa somo kutoka Zaburi 39 "Nalisema nitazitunza njia zangu nisije nikakosa kwa ulimi wangi", Pambo alijibu: "Hii inatosha kwa leo". Akaenda jangwani kufikiri juu ya maneno hayo. Alipomaliza

kutafakari juu ya meneno hayo kwa miezi sita, alirudi tena kuendelea na masomo yake.

Mt. Melania mjane aliyefungua nyumba ya kitawa huko Yerusalemu, alimtembelea Mt. Pambo, na kumletea zawadi ya pauni mia tatu za sarafu. Alipozipokea, alisema kuwa zingeweza kutumika kwa ajili ya Monasteri maskini, lakini hakushukuru. Melania alimkumbusha kwa upole: "Kuna pauni mia tatu za sarafu, baba yangu". Yule uliyemtolea zawadi hii, hana lazima yako wewe umwambie ina thamani gani". Na wakati mwingine alipoombwa ahesabu fedha aliyopewa ili akaigawe, alisema: "Mungu haulizi ni kiasi gani, bali zimetolewaje na kwa nia gani".

Pambo alifariki akiwa anasuka kikapu. Alisema: "Tangu nilipokuja jangwani, sijala chochote ambacho sijakifanyia kazi, na sikumbuki kama hata mara moja nilisema kitu chochote ambacho nilikisikitikia baadaye". Mt. Melania alikuwepo alipokufa; alikuwepo pia kwenye mazishi yake, na akachukua kikapu kilichokuwa kinashonwa na Mt. Pambo kama mabaki ya thamani kubwa.

*MT. PAMBO, UTUOMBEE*

*MASOMO YA MISA*

I. Kut. 1:8-14,22

Zab. 124

INJILI. Mt. 10:34-11:1