Catholic Diocese Malindi

slider10.jpg
slider5.jpg
slider8.jpg
slider6.jpg
slider11.jpg
slider9.jpeg
previous arrow
next arrow

*MAISHA YA WATAKATIFU*

*MT. HENRI (HENRIKO),* KAISARI WA UJERUMANI
( 13 JULAI )

Henri alizaliwa Regensburg mkoani Bavaria (Ujerumani) mwaka 973. Mtakatifu Wolgang, Askofu wa Regensburg, alimlea katika ibada na uchaji wa Mungu. Baba yake alipokufa, alirithi nchi ya Bavaria, akamwoa mke, jina lake Kunegunda.

Miaka kadhaa baada ya hayo, Henriko alichaguliwa kuwa mfalme wa Ujerumani. Tangu siku ile, alifanya bidii kuistawisha dini Katoliki katika nchi zake. Aliyajengesha upya Makanisa mengi yaliyoharibiwa na maadui wa dini, alimrudisha Roma Papa Benedikto wa Nane, aliyefukuzwa na papa wa uwongo. Baba Mtakatifu naye alimwita aje Roma, akamvika kichwani taji la Ukaisari, kama tuzo kwa kazi zake njema za kumkinga Papa.

Kaisari Henriko, siku zote aling'amua hatari zinazowanyemelea watu wanaokuwa katika madaraka makubwa. Kwa kusali, aliweza kushika moyoni mwake fadhila za unyenyekevu na uchaji wa Mungu alizohitaji maishani mwake. Alifanya bidii kubwa kuleta amani na furaha katika milki yake, akasaidia kuwaongoa watu wa Hungaria wawe Wakristo.

Alijenga Kanisa kuu na Monasteri mjini Bamberg. Kisha akaweka akiba fedha nyingi sana kwa ajili ya Makanisa na maskini viweze kuendelea mpaka mwisho wa nyakati. Alikufa mwaka 1024, akatangazwa kuwa Mtakatifu mwaka 1146.

*MT. HERNIKO, UTUOMBEE.*

*MASOMO YA MISA*

I. Mwa. 44:18-21,23-29; 45:1-5

Zab. 105:16-21

INJILI. Mt. 10:7-15