slider10.jpg
slider5.jpg
slider8.jpg
slider6.jpg
slider11.jpg
slider9.jpeg
previous arrow
next arrow

_*Mtakatifu Alphonsus Rodriguez*_

Mtakatifu Alphonsus Rodriguez alizaliwa tarehe 25 Julai 1532 huko Segovia, Hispania. Baba yake alikuwa mfanyabiashara.

Alisoma katika shule ya wa Jesuit huko Alcala, lakini akarudi nyumbani kutokana na kifo cha baba yake. Akiwa Segovia, aliamua kufanya biashara, ambayo baba yake alikuwa akifanya.

Alioa, akapata watoto watatu.Lakini watoto hao wote walikufa katika vipindi tofauti.Baadae mke wake pia alikufa.

Mtakatifu Alphonsus aliamua kuuza biashara zake, na akaomba kujiunga na shirika la wa Jesuit. Lakini hakukubaliwa ,kutokana na Kiwango chake kidogo cha elimu,na udhaifu wa afya yake.

Lakini mwaka 1571 Januari 31 ,alipokelewa na shirika la wa Jesuit, kama Brother, mlei. Akapewa mafundisho mbalimbali, kisha akatumwa kufanya kazi katika kisiwa cha Majorca.

Hapo alifanya kazi kama mbeba mizigo katika chuo cha wa Jesuit cha Montesion kwa miaka 20.Akawa rafiki wa kila mtu, akiwa mnyenyekevu.Akashauri wanafunzi, pamoja na watu waliokuwa hapo kwa busara Na nyakati zingine akaandika nyaraka tofauti za mafundisho.

Mtakatifu Alphonsus alikufa tarehe 31 October 1617.Alitangazwa mwenye heri mwaka 1825, na mwaka 1888 akatangazwa Mtakatifu.

*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Wolfgang
Mt. Abaidas
Mt. Antoninus
Mt. Arnulf
Mt. Bega
Mt. Erth
Mt. Notburga
Mt. Quentin

*Mtakatifu Alphonsus, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, _Mtuombee......🙏_*