slider10.jpg
slider5.jpg
slider8.jpg
slider6.jpg
slider11.jpg
slider9.jpeg
previous arrow
next arrow

*KUPALIZWA BIKIRA MARIA MBINGUNI*

( 15 AGOSTI )

Leo hii Kanisa linafurahia kutukuka kwake mtumishi mnyenyekevu wa Bwana. Ni sikukuu kubwa kupita zote zinazoadhimishwa na Kanisa kwa heshima yake. Kanisa Katoliki hufundisha kwamba Bikira Maria ambaye alihusiana kwa karibu sana na Kristo Mwanae katika mafumbo ya wokovu, alipalizwa mbinguni roho na mwili, na sasa hushiriki ushindi na heri yake. Tangu karne ya Tano, Wakristo wamesadiki kabisa kwamba mwili wake Bikira haukuoza kaburini, na Sikukuu ya Kupalizwa kwake

imesherehekewa tangu karne ya sita. Mnamo mwaka 1950, Papa Pius wa Kumi na Mbili baada ya kuwahakikishia Maaskofu wa Kanisa zima, alitangaza kwamba fundisho hilo ni moja ya mafundisho makuu ya Imani Katoliki.

Fundisho hili hutueleza kwamba hatuna budi kuuthamini mwili wa kibinadamu ambao baada ya ubatizo ni Hekalu la Roho Mtakatifu, na mwisho wa nyakati utafufuliwa kaburini. Ndipo wakombolewa wote watakuwa wanaishiriki, mwili na roho, heri ya mbinguni. Bikira Maria amewatangulia na kuishiriki sasa hali hiyo ambayo tumetayarishiwa sisi sote.

Papa, wakati ule alipotangaza rasmi fundisho hilo, aliandika: "Ufufuko wa Bwana wetu ulikuwa utukufu wa ajabu na tukio lenye kusababisha ushindi mkuu juu ya dhambi na mauti; na Bikira Maria aliyeshiriki mapigano hayo, lazima ashiriki ushindi huo katika kutukuka kwa mwili wake wa Kibikira".

*Mama Yetu Maria, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, _Mtuombee.....🙏_*