Mhashamu Baba Askofu Willybard Lagho, Askofu wa Jimbo Katoliki la Malindi, alijumuika na watoto wa PMC kutoka Parokia ya Tarassa katika hafla maalum ya kuadhimisha umoja wao. Ibada ya misa iliongozwa na Baba Askofu na katika mahubiri akasitiza umuhimu wa kuwa na nidhamu katika maisha yao ya kila siku.
Baada ya ibada ya misa, Askofu Lagho aliwazawadi watoto kama ishara ya upendo na kutambua juhudi zao katika kuishi imani yao ya kikatoliki. Vilevile, alijumuika nao katika burudani na michezo, akionyesha mshikamano na furaha kwa watoto hao wa PMC.
Katika ujumbe wake kwa watoto, Mhashamu Baba Askofu, Willybard Lagho alisisitiza umuhimu wa nidhamu kama nguzo muhimu katika maisha ya Kikristo. Alikazia pia umuhimu wa kusoma na kuzingatia mafundisho ya Kanisa, akiwahimiza watoto kuhudhuria mafundisho ya dini na kufuata maagizo ya viongozi wa Kanisa ili kuishi maisha bora ya kiroho. Aliwahimiza kuwa mfano wa wema na uaminifu kwa familia zao na kwa jamii kwa ujumla.