Catholic Diocese Malindi

slider10.jpg
slider5.jpg
slider8.jpg
slider6.jpg
slider11.jpg
slider9.jpeg
previous arrow
next arrow

ASALI MUBASHARA-Alhamisi 01/06/2023

Bila Yesu, sisi ni Vipofu

Ndugu zangu wapendwa karibuni kwa adhimisho la misa takatifu. Bartimayo baada ya kuambiwa kuwa ni Yesu Mnazareti anapita katika njia ile; anapaaza sauti yake

“Yesu Mwana wa Daudi unirehemu.” Maneno haya ni aina ya sala tunayoiita “Sala ya Yesu.” Ni sala tunayopaswa kuisali kila mara; ni sala ambayo tunaweza kuisali kwa uaminifu wakati tunapokubali kwamba sisi tunahitaji msaada wa Yesu.

Maelezo ya yule kipofu ni maneno ambayo yanamfaa kila mmoja wetu anayemtambua Yesu. Sisi bila Yesu, ni vipofu, hatuwezi kuona vizuri. Sisi ni waombaji.

Tunaweza kumfuata Yesu kweli kama tutatambua kwamba, hata tuwe na akili au mali nyingi kiasi gani, sisi kwa hakika ni maskini. Yule kipofu alikuwa amekaa kando ya barabara, sio barabarani. Na hii ndio maana halisi ya anaye kaa kando ya barabara, kwamba ni mwombaji na kipofu kweli.

Barabara au njia ni ishara kwamba Kristo ni njia, ukweli na uzima wote (Yn 14:6). Ujumbe ni kwamba baada ya kipofu kukutana na Yesu sasa anaweza kuona tena na anafuatana na Yesu barabarani. Nasi tuliokutana na Yesu katika ubatizo, tutembee katika njia yake.

Sala: Yesu Mpendwa, naomba niweze kuona vyema, Amina.

©️Pd. Prosper Kessy OFMCap.