slider10.jpg
slider5.jpg
slider8.jpg
slider6.jpg
slider11.jpg
slider9.jpeg
previous arrow
next arrow

*ASALI MUBASHARA –Jumamosi 4/11/2023*

Karibuni ndugu zangu kwa adhimisho la Ekaristi Takatifu asubuhi ya leo.

Leo neno la Bwana katika asubuhi ya leo tunaanza kwa kuliangalia somo la kwanza linalotoka katika barua ya mtume Paulo kwa Warumi. Hapa tunamkuta Paulo akigeuza kibao-jana alikuwa ameongea kwa uchungu sana juu ya wana wa Israeli kukataa kumpokea Yesu kama Masiha wao na kuwasifu watu wa mataifa jinsi walivyompokea Yesu na kupata wokovu, sasa leo anasema kwamba licha ya hayo yote waliyofanya na kutenda, bado wana Waisraeli wanazidi kubakia kuwa wateule wa Bwana, na anasema kwamba si wote wataangamia bali Mungu amejitengea watu wake kati ya hao wana wa Israeli ambao watamsikiliza na kulifanya agano lake litimie bila kuonekana kama limeshindwa.

Hawa ndugu zangu ni wale Wayahudi watakaompokea Kristo. Na hawa wataifanya dunia ibarikiwe maradufu kwa sababu kama kitendo cha Wayahudi kuikataa Injili kilisababisha watu wa mataifa wafaidike, yaani injili ihubiriwe kwao badala ya Wayahudi na hivyo kuokoka, Paulo anasema kwamba watakapo mpokea Kristo hawa Wayahudi, baraka zitaongezeka Zaidi hata kwa watu wa mataifa kwani ikiwa kukataa kwao injili kulileta faida hivi, kadhalika kuikubali kwao Injili kutasababisha maendeleo makubwa.

Injili ya leo inakamilisha ujumbe huu kwa mapana zaidi kwa kuonyesha kwamba kinachotakiwa hapa ni kila mtu kuelewa nafasi yake na kubakia katika hiyo nafasi yake. Wana wa Israeli walijivuna wakijiona kwamba ni taifa teule, wakaenda kukaa sehemu za mbele wakijiona kwamba sherehe ni yao lakini alipokuja Bwana wa harusi aliwatimua na kuwatupa kwenye viti vya nyuma. Watu wa mataifa walionyesha unyenyekevu, walikaa siku zote viti vya nyuma (kama yule mama Mkananayo aliyeambiwa na Yesu si vizuri kuwalisha chakula cha watoto mbwa) na Yesu alipokuja aliwatoa huko. Hata hawa watu wa mataifa wanapaswa waendelee kuonyesha unyenyekevu kwani nao wakijidai kuendelea kujiona kwamba wao wanastahili viti vya mbele watakuja kutimuliwa huko tu.

Hapa ndugu zangu tunajifunza mengi: kwanza-unyenyekevu ndio utakaokuokoa. Unapokuwa umepewa cheo au nafasi fulani, ukijiona kwamba hustahili na hivyo ukiendelea kufanya bidi kwa nguvu, utashinda tu. Lakini utakapojiona unastahili na kuanza kulala tu, huu ndio mwanzo wa maanguko.

Kingine: unapokuwa kwenye kitu cha mbele, kuna ile kasumba ya kujisahau, kujiona kana kwamba wewe ni mafia, kila kitu na mwishowe unakuwa mzembe na unaharibu kila kitu. Hili ni fundisho kwa wote wenye vyeo na mabosi. Angalieni inawezekana kwamba hivyo vyeo vyenu vyaweza kuwa mwanzo wenu wa kuanguka na kuporomoka chini kabisa.

Unapokuwa umekaaa katika nafasi ya nyuma, kunakuwaga na ile hali ya kujihangaisha ili uone mbele, kujishughulisha, ni muhimu sana. Hivyo, unakuwa unasogea taratibu mbele.

Halafu, kwa wale wenye pesa, utajiri, nafasi nzuri kazini, na watoto wa wenye nazo. Angalia sana. Usipokazana na kuishi kama siku zote umekaa mbele karamuni, keshokesho tu utakuwa maskini. Hivyo, pale ulipo jishughulishe. Hata wewe mtoto wa tajiri, jishughulishe. Tambua yote ni ya Mungu na tumia kwa unyenyekevu kwa ajili ya wengine pia. Usijikweze, Mungu ataviondoa, awape watu wamataifa.

©️Pd. Prosper Kessy OFMCap.