CWA at the Seminar in Muyeye Parish

CWA-Muyeye wafanya semina juu ya wajibu wa mama katika kanisa la familia, jumuiya ndogondogo na parokia kwa mfano wa Maria Mama wa Yesu.

Semina hiyo ilifanyika siku ya jumamosi ya tarehe 11 Machi 2023 katika ukumbi wa parokia ikiongozwa na Pd. Damas Missanga, S.J., msaidizi wa paroko. Pd. Missanga alisema kuwa wajibu wa mama katika kanisa unaangaliwa kwa mfano wa Mama Maria aliye mfano wa wanawake wote. Maria aliyekuwa Mwanamke wa Imani, Mwanamke wa sala, mtii, mnyenyekevu, msaidizi, mvumilivu, mlezi, imara, mfuasi wa karibu wa Yesu na asiyekata tamaa kamwe.

Kila mwanamke aliaswa kujipima kila mara kwa vigezo vya Mama Maria na kuona ni wapi alikofanikisha na wapi bado ili aweze kuongeza juhudi zaidi katika hilo.

Aliongeza kusema kuwa ufanisi hafifu au kutofanikiwa kabisa katika baadhi ya vigezo si sababu ya kukata tamaa bali ni chachu na sababu nzuri ya kutafuta msaada kwa Mama katika sala na sakramenti mabimabli zitolewazo na kanisa. Kutokujaribu ni kutokujua yalipo mafanikio na mapungufu na hivyo kukosa mpango-sala tiririshi wa shukrani au maombi.