Zawadi Ya EID Kwa Kina Mama Waislamu

Jimbo katoliki la Malindi, tarehe ishirini mwezi wa April mwaka huu liliandaa zeozi la ugavi wa chakula kwa kina mama ishirini kutoka kwa familia zisizojiweza za kiislamu. Familia hizi ni pamoja na watoto hamsini na waili kutoka kwa familia hizo.

Ni zoezi lililofanyika katika Catholic Institute. Zoezi hili liliongozwa na Ciara anayefanya kazi na shirika la inter-religious dialogue katika jimbo katoliki la Malindi.

Akizungumza na Radio Bayana wakati wa kugawanya chakula hicho, Ciara anasema lengo kuu la zoezi hili ni kuonyesha upendo baina ya wakristu na waislamu hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan na pia wanapokamilisha mfungo huu.

“Tumeandaa mpango huu kama njia ya kuonesha ushirikaino mwema na baina ya wakristu na waislamu hasa kuwapatia msaada wa chakula katika mwezi huu mtuku wa Ramadhan na pia wanakapoisherehekea Eid.”

Aidha Ciara alisema majina ya familia hizo yalipeanwa na viongozi wa dini ya kiislamu na wanafurahia kwa kuwasaidia kwani kwasasa bei za bidhaa ziko juu humu nchini.

“Tulipewa majina ya familia hizi na viongozi wa kiisalamu ambao tunaushirikiano nao na tumefurahia kuwasaidia kwani kwasasa humu nchini bei za bidha iko juu mno”, Ciara alisema.

Wanafamilia waliopokea msada huo, wakiongozwa na Amina Salim, anasema wanafurahia kwa Jimbo Katoliki la Malindi kuwatunuku zawadi ya Eid.

“Mungu azidi kulibariki jimbo katoliki la Malindi kwa kusimama na sisi wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Wameonyesha upendo wa dhati kwa kutuzawadi wakati huu ambapo tunamaliza mfungo wa Ramadhan ili kusherehekea Eid. Hatua hii itadumisha ushirikiano mwema katika ya wakristu na wailsamu, tunashukuru sana”, Amina alisema.